Sexe Model huren porn tube

Mwongozo wa maungamo mazuri

Hitaji la msingi katika maungamo mazuri ni kuwa na nia ya kurudi kwa Mungu kama Mwana Mpotevu, na kukubali dhambi zetu kwa sikitiko la kweli mbele ya padre, mwakilishi Wake.

KABLA YA MAUNGAMO

Uwe kweli umechukizwa na dhambi. Tendo muhimu la Kitubio, kwa upande wa mwenye dhambi, ni majuto, kukiri kwa uwazi dhambi iliyofanyika pamoja na azimio la kutofanya tena, kwa sababu ya upendo ulio nao kwa Mungu. Kwa uelewa huu basi, majuto ni mwanzo na moyo wa uongofu ambao humleta mtu kurudi kwa Mungu kama Mwana Mpotevu anavyorudi kwa baba yake, na ndiyo ishara wazi
ionekanayo ya Sakramenti ya Kitubio. Azimio la kuepuka kufanya dhambi hizi katika siku zijazo (kujirekebisha) ni ishara kuwa majuto yako ni ya kweli na ya uhakika. Hii haimaanishi kwamba mtu kamwe hatatenda dhambi tena. Ni azimio la kujaribu kuzuia mazingira ya karibu yanayokurudisha tena dhambini. Neema ya Mungu ikishirikiana na nia ya kurekebisha maisha yako, itakupa nguvu ya kupinga
na kushinda majaribu katika siku zijazo.

KUCHUNGUZA DHAMIRI

Chunguza dhamiri yako. Kumbuka dhambi zako. Kwa utulivu jiulize kile ulichokifanya kwa uelewa na ridhaa kamili dhidi ya Amri za Mungu.

AMRI YA KWANZA
 Nimetimiza nyadhibu zangu kwa Mungu kwa kusuasua ama kwa kinyongo?
 Je, nilidharau maisha yangu ya sala? Je, nimesali sala zangu za kila siku?
 Je! Nimepokea Komunyo Takatifu katika hali ya dhambi ya mauti au bila maandalizi ya lazima?
 Je, nimefunga lisaa kabla ya kupokea Ekaristi?
 Je, nilishindwa kutaja dhambi kubwa katika maungamo yangu yaliyopita?
 Je, nimeamini katika ushirikina au kujiingiza kwenye vitendo vya kishirikina (kusoma viganja, kubashiria bahati, nk.)?
 Je, nilikuwa na mashaka makubwa juu ya Imani?
 Je, nimeweka imani yangu katika hatari, bila sababu nzuri, kwa kusoma kitabu, jarida, au gazeti lililo na nyenzo kinyume na imani Katoliki au maadili?
 Je, nimehatarisha imani yangu kwa kujiunga au kuhudhuria mikutano ya mashirika yanayopinga imani Katoliki (kupambana na kanisa Katoliki, Chama cha Kikomunisti, Freemasoni, ibada au dini nyingine)? Je! Nimeshiriki katika moja ya shughuli zake?
 Je, nimefanya dhambi ya kukufuru utakatifu (mtu, mahali au kitu)?

AMRI YA PILI
 Je, nimeshindwa katika jitihada zangu kutimiza ahadi na maazimio niliyoyaweka kwa Mungu?
 Je, nimetumia jina la Mungu bure? Nimetumia jina la Mungu katika matani, hila, hasira, au kwa sababu nyingine yoyote isiyo na maana?
 Je, Nimelitaja jina la Bikira Maria au jina la Mtakatifu mwingine kwa dharau, kwa kuchukiza, kwa hasira, au namna isiyo ya kawaida?
 Je, nimekuwa msimamizi wa Ubatizo au kushiriki kikamilifu ibada nyingine nje ya Kanisa Katoliki?
 Je, nimeshasema uongo wakati wa kiapo? Je, nimeshavunja ahadi nilizoweka (binafsi au hadhrani)?
 Je, nimetumia lugha mbaya?

AMRI YA TATU
 Je, nimekosa Ibada Takatifu Dominika au siku zilizoamriwa?
 Je, nilishindwa kuvaa ipasavyo kwenye Ibada Takatifu?
 Je, bila sababu ya kutosha, nimechelewa Ibada Takatifu ya Misa au Kushindwa kuhudhuria Misa Jumapili au siku takatifu iliyoamriwa?
 Je! nimekuwa sio mtulivu wakati wa Misa, kutofuatilia Misa na kuangalia huku na huko nk?
 Je, nimefanya mtu mwingine kuwa na wasiwasi?
 Je, nimefanya kazi yoyote au biashara ambayo imekuwa kizuizi katika kumwabudu Mungu, siku ya furaha inayofaa, siku ya utulivu sahihi kwa kupumzisha akili na mwili, Dominika au siku takatifu iliyoamriwa?
 Je, nimeshindwa kutoa kwa ukarimu kulisaidia Kanisa katika mahitaji yake kwa kiwango ambacho nina uwezo?
 Je, nimeshindwa kufunga au kushika kitakatifu siku iliyowekwa na Kanisa?

AMRI YA NNE
KWA WAZAZI
 Je, nimeacha kuwafundisha sala watoto wangu, kuwapeleka kanisani, ama kuwapa elimu ya Kikristo?
 Je, nimewapa mfano mbaya?
 Je, nimeshindwa kuwalea watoto wangu, kufuatilia aina za marafiki zao, vitabu  wanavyosoma, sinema, maonyesho ya televisheni, michezo ya video na tovuti za mitandao wanazoziangalia?
 Je, nimeshindwa kuona kwamba watoto wangu wamepokea Sakramenti ya Kitubio na Komunio ya kwanza?
 Je, nimeshindwa kuona kwamba watoto wangu wamepokea Sakramenti ya Kipaimara?
 Je, nimekosa utii kwa wazazi wangu au wakuu wangu halali katika mambo muhimu?

KWA WATOTO
 Je, nimekuwa mtii kwa wazazi wangu?
 Je, nimeacha kuwasaidia wazazi wangu pale walipohitaji msaada wangu?
 Je, nimeshindwa kuwapenda wazazi wangu au kuwaheshimu?
 Je, nimekuwa na majigambo pindi niliporekebishwa na wazazi wangu?
 Je, nimekuwa na mwelekeo mbaya wa uhuru?
 Je, nimetimiza wajibu wangu?

AMRI YA TANO
 Je, nimekuwa mtu wa hasira sana?
 Je, nimekuwa na wivu kwa wengine?
 Je, nimejeruhi au kukatiza maisha ya mtu yeyote? Je, nimeendesha gari bila tahadhari? 
 Je, nimekuwa sababu ya wengine kuanguka dhambini katika mazungumzo, kusema utani, ubaguzi au udhalilishaji, namna ya kuvaa, kumkaribisha mtu kuhudhuria maonyesho ya matukio fulani yasiyofaa, kuazima vitabu au magazeti yasiyofaa, kusaidia mtu kuiba, nk? Je, nimejaribu kurekebisha vikwazo hivyo?
 Je ni watu wangapi nimewaangusha dhambini? Ni dhambi zipi zimehusika?
 Je, nimepuuza afya yangu? Je, Nimejaribu kukatiza maisha yangu?
 Je, nimejikata viungo ama kuwakata wengine?
 Je, nimekuwa mlevi au kutumia dawa za kulevya?
 Je, nimekula au kunywa zaidi ya kiasi, kiasi cha kuwa mlafi?
 Je, nimeshiriki katika aina yoyote ya ukatili dhidi ya mwili?
 Je, nimekubali kwa hiari au kushiriki kikamilifu katika njia za uzazi wa mpango za utasa? (kufunga kizazi, kukata mirija n.k)? Je, ninatambua kwamba hili litakuwa na athari ya kudumu kwenye maisha ya ndoa na kwamba nitahitaji kutoa majibu kwa Mungu kwa matokeo hayo?
 Je, nimekubali kwa hiari yangu, kushauri, au kushiriki kikamilifu katika kutoa mimba? Je, natambua kwamba Kanisa linaadhibu moja kwa moja kwa kuwatenga (latae sentenciae) wale wanaohusika kutoa mimba? Je, natambua kwamba hili ni kosa kubwa sana?
 Je, nimemwumiza mtu yeyote kwa maneno au matendo yangu?
 Je, nimetamani kulipiza kisasi au kuweka uadui, chuki, au hisia mbaya pale mtu anaponikosea?
 Je, nimeomba msamaha pale nilipomkosea yeyote?
 Je, nimekataa kusamehe?
 Je, nimewatukana wengine au kuwachukiza?
 Je, nimegombana na mmojawapo wa ndugu zangu?

AMRI YA SITA NA YA TISA
 Je, kwa kudhamiria niliwaza machafu?
 Je, nilikubali tamaa mbaya zinazopingana na usafi wa moyo, hata kama inawezekana sikuzitekeleza? Je, kulikuwa na mazingira yoyote yaliyoifanya dhambi hiyo kuwa kubwa sana? (kwa mfano uhusiano wa damu, iwe ni kwa aliyeolewa/oa au kwa anayeishi maisha ya wakfu kwa Mungu?
 Je, nimejiingiza katika mazungumzo machafu? Niliyaanzisha mimi?
 Je, nimetafuta starehe katika aina fulani za burudani zilizonifanya nikaribie kutenda dhambi, kwa mfano aina fulani za kucheza, maigizo, sinema, au hata vitabu ambavyo vina matendo yasiyofaa kimaadili? Je, nimetembelea majumba au kuwawahifadhi marafiki wasio na maadili?
 Je, nilimbua kuwa ninaweza kuwa nimeshatenda dhambi kwa kujiweka katika mazingira ya kuanguka dhambini, kwa mfano kwa kushirikiana chumba na mtu ninayemtamani kimapenzi, au kuwa peke yangu na mtu ambaye ninamtamani kimapenzi au mazingira ambayo yanaweza kurahisisha kukamilisha dhambi ya kuzini?
 Je, nilishindwa kujisitiri vizuri katika kuulinda usafi wa moyo?
 Nilishindwa kuchukua tahadhari, kabla ya kwenda kuangalia sinema ama kusoma kitabu; kuona kama kinafaa kimaadili ama la, ili kutojiweka katika mazingira ya kutenda dhambi ama kuharibu dhamiri yangu?
 Kwa kudhamiria, nilitazama picha zisizofaa (aina yoyote ya picha za utupu) au kujitazama kwa tamaa au kuwatazama wengine kwa tamaa? Nilidhamiria mwenyewe kutenda dhambi ya kuzini?
 Niliwaongoza wengine kwenye dhambi za uchafu au uasherati? Dhambi zipi haswa walitenda?
 Nilifanya tendo chafu? Peke yangu, kwa kujichua (masturbation) ambayo ni dhambi ya mauti; nilifanya na mtu mwingine? Mara ngapi? Mtu huyo alikuwa wa jinsia tofauti ama jinsia mfanano? Kulikuwa na mazingira yoyote ya kuashiria uhusiano wa damu ambao ungesababisha dhambi iwe kubwa zaidi? Uhusiano huu usiokubalika kisheria ulipelekea mimba? Nilifanya chochote kujaribu kuzuia ama kuudhuru ujauzito huo?
 Je, nina marafiki ambao wana tabia ya kutenda dhambi za uchafu? Je, nimeshajiandaa kuachana nao?
 Katika uchumba, ni upendo wa kweli unanisukuma niwe na mwenza? Je, ninaishi hali ya kawaida na ya kujitoa sadaka ili kutomweka mwenza wangu katika hatari ya kutenda dhambi?
Ninachanganya upendo wa kweli kwa binadamu na upendo wa kihisia, kichoyo na wa kujitakia anasa tu?
 Je, nimeshiriki vitendo kama vya kushikana, mabusu ya kimahaba, au kukumbatia kimahaba kwa muda mrefu?
KWA WATU WALIO KATIKA NDOA
 Je, nimemnyima mwenzangu wa ndoa haki ya tendo la ndoa pasipo sababu maalumu?
 Je, nimejitafutia haki yangu pekee, pasipo kuonesha kujali haki ya mwenza wangu na hali yake kiakili na kimwili? Je, nimesaliti uaminifu wa ndoa kwa tamaa ama kwa matendo?
 Je, nimetumia vidonge vya uzazi wa mpango au kifaa mfanano kabla au hata baada ya kugundua utungisho ulikwishatokea?

 Je, nipo wazi kuruhusu uhai kama zawadi ya Mungu kwa wanandoa?
 Je, nimemshawishi mtu yeyote kutumia vidonge vya uzazi wa mpango au kutumia njia nyingine za kisasa za kuzuia mimba (mfano kutumia kondomu).
 Je, nimeshiriki katika kusababisha watu kuwa na mawazo ya kutumia vizuizi mimba; kwa ushauri, utani, au mtizamo? (juu ya utoaji mimba, vizuizi mimba, kufunga uzazi, n.k – tazama maelezo katika Amri ya Tano).

AMRI YA SABA NA YA KUMI
 Je, nimeiba? Je, kiasi gani cha fedha? Au nilichoiba kina gharama gani?
 Je, nimerudisha nilichoiba? Au walau nimekuwa na wazo la kurudisha?
 Je, nimekuwa sababu au nimesababisha uharibu wa mali ya mtu mwingine? Kwa kiwango gani?
 Je, nimemuumiza yeyote kwa udanganyifu, utapeli katika bishara, mikataba au miamala ya fedha?
 Je, nimetumia zaidi ya kile ninachoweza kukipata? Ninatumia pesa nyingi kwa mambo yasiyo na msingi ya ulimwengu huu tuu (kipuuzi)?
 Je, nimetoa kwa wahitaji (sadaka) kwa kiasi ninachopaswa kutoa kulingana na hali yangu?
 Je, nimekuwa na wivu na mali ya jirani yangu?
 Je, nimepuuzia mbali kutaka kulipa madeni ninayodaiwa?
 Kwa kujua, nimepokea mali ya wizi?
 Je, nimetamani kuiba?
 Je, nimependelea uvivu au kupenda kuburudika zaidi, badala ya kufanya kazi kwa ustaarabu au kusoma?
 Je, nimekuwa na tamaa? Je, ninaona muono mzima wa maisha katika mali zaidi?

AMRI YA NANE
 Je, nimesema uongo? Nimefanya malipizi kwa hasara yoyote iliyojitokeza kutokana na kusema kwangu uongo?
 Je, nimewashutumu au kuwafanyia jeuri wengine bila haki, tena watu wasio na hatia?
 Je, nimetenda dhambi ya kusema makosa ya wengine pasipo na ulazima? Je, nimetenda dhambi ya kuwasingizia wengine/kuwasema wengine mambo ambayo si ya kweli?
 Je, nimejiingiza katika umbeya na uzushi?
 Je, nimetoa siri pasipo sababu linganifu (ya msingi)?

Kama una swali lolote waweza kumuuliza Padre. Kisha ongeza: Ninaomba msamaha kwa makosa haya na makosa mengine ya nyuma nisiyoyakumbuka. Padre atakupa kitubio na kukupa ushauri utakaokusaidia kuwa Mkristo mwema. Sikiliza maneno ya Padre na uwe tayari kutekeleza kitubio haraka iwezekanavyo. Kitubio kitamaliza adhabu za muda zitokanazo na dhambi zilizosamehewa.

SALA YA KUTUBU

Ee Mungu wangu, ninaumia moyoni kwa makosa niliyokutendea, na ninadhamiria kuziacha dhambi zangu zote, kwa sababu naogopa kupoteza kuiona mbingu na kupata maumivu ya jehanam; lakini zaidi kwa sababu dhambi zinakuchukiza, Mungu wangu, ambaye ni Mzuri daima na unayepaswa kupendwa nami kwa moyo wote. Ninadhamiria kwa ari moja, kwa msaada wa neema yako, kuziungama dhambi
zangu, na kubadili mfumo wa maisha yangu. Amina.
Au Mungu wangu, ninasikitika kwa dhambi zangu moyoni mwangu. Katika kuchagua kutenda baya na kushindwa kutenda jema, nimekukosea Wewe, ambaye napaswa kukupenda kuliko chochote.
Ninadhamiria kwa nia moja, kwa msaada wako, kufanya kitubio, kutokutenda dhambi tena, na kuepuka chochote kitakachonipeleka dhambini. Mkombozi wangu Yesu Kristo, uliteseka na kufa kwa ajili yangu, Nionee huruma. Amina.
Sikiliza maneno ya maondoleo ya dhambi kwa makini. Fanya ishara ya Msalaba na mwishoni itikia:
Amina.
BAADA YA MAUNGAMO
 Mshukuru Mungu kwa kukusamehe dhambi tena.
 Kwa muda muafaka na kwa unyenyekevu timiza kitubio/malipizi uliyopewa na Padre. Ingawa unaweza kupokea Komunyo Takatifu hata kabla ya kutimiza malipizi, inashauriwa kufanya malipizi mapema iwezekanavyo.
 Kama ukikumbuka dhambi kubwa ambayo ulisahau kuiungama, amini kwamba
ilikwishasamehewa na zile nyingine, lakini hakikisha unaisema katika maungamo yajayo.
 Ishi maisha ya kuwa Mkristo Mkatoliki Mwema, Mtakatifu na mwenye Furaha.

Kwa wale ambao wamekuwa mbali na Sakramenti ya Upatanisho na msamaha wa upendo, nashauri haya: Rudi kwa chanzo hiki cha neema; usiogope! Kristo mwenyewe anasubiri kwa ajili yako. Yeye atakuponya, na utakuwa na amani na Mungu! (Yohana Paulo II)

Pridaj komentár

Vaša e-mailová adresa nebude zverejnená. Vyžadované polia sú označené *