Sexe Model huren porn tube

Njia ya msalaba na Mt. Faustina

Kufuatana na Shajara ya Mt. Faustina Huruma ya Mungu Rohoni Mwangu

Sala ya Utangulizi:
Yesu wa Huruma, Bwana wangu, natamani kukufuata kwa uaminifu na kukuiga kila siku kwa ukamilifu zaidi. Kwa sababu hii nakusihi kwamba, kwa njia ya kuyatafakari mateso yako, niweze kupokea kila siku neema ya kuelewa kwa ukamilifu zaidi, mafumbo ya maisha ya kiroho.
Maria, Mama wa Huruma, daima mwaminifu kwa Kristo, uniongoze kupitia hatua za mateso na huzuni ya Mwanao na nijaliwe neema muhimu ili njia hii ya msalaba iweze kuwa na matunda moyoni mwangu.

KITUO CHA KWANZA: Yesu Anahukumiwa Afe.
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Usishangae kwamba wakati mwingine utashitakiwa bila kosa. Mimi mwenyewe ni kwanza kukinywea kikombe hiki cha mateso nisiyostahili kwa ajili ya upendo wangu kwako. (289). Nilipokuwa mbele ya Herode, nilipata nee ma kwa ajili yako, kwamba utaweza kuinuka juu ya dharau ya mwanadamu na kufuata kwa uaminifu nyayo zangu. (1164).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu, tuna uharaka wa maneno na twataka kujibu kwa haraka, bila kutathmini kama ndio mpango wa Mungu kwamba tunapaswa kusema. Nafsi iliyo na ukimya ina nguvu: Haikumbwi na madhara pindi ivutapo Subira katika ukimya. Ina uwezo wa kufikia Muungano wa karibu na Mungu. (477).
Yesu wa Huruma, nisaidie nikubali kila hukumu ya mwanadamu; usiniruhusu kamwe nikuhukumu wewe ninapohukumu jirani yangu.

KITUO CHA PILI: Yesu Anabeba Msalaba
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Usiogope mateso, nipo pamoja nawe, (151). Kadiri utakavyozidi kuyapenda mateso, ndivyo hivyo mapendo yako safi Kwangu yatakavyokuwa. (279).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu, nakushukuru kwa misalaba midogo ya kila siku, kwa kupinga mipango yangu, kwa ugumu wa maisha ya kijamii, kwa tafsiri mbaya ya nia zangu, kwa fedheha mbele ya wengine, kwa ukatili tunaotendewa, kwa tuhuma za uwongo, kwa afya mbaya na kupoteza nguvu, kwa kujikana mwenyewe, kwa kufa kwangu mwenyewe, kwa kutotambuliwa katika kila kitu, kwa kuharibika kwa mipango yangu yote. (343).
Yesu mwenye huruma, nifundishe kuthamini ugumu wa maisha, magonjwa, mateso, na kwa upendo chukua msalaba wangu wa kila siku.

KITUO CHA TATU: Yesu Anaanguka kwa Mara ya Kwanza.
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Makosa yasiyo hiari hayazuii upendo Wangu kwa watendao au kunizuia Mimi kujumuika nao. Lakini makosa ya hiari, huzuia neema Yangu, na siwezi kutoa zawadi Zangu kwa roho kama hizo. (1641).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu wangu, jinsi gani ninavyoathirika na uovu, na hii inanilazimu kuwa macho kila wakati. Lakini sikati tamaa. Ninaamini neema ya Mungu, inayozidi hasa katika shida kubwa zaidi. (606).
Bwana mwenye Huruma, kwa hiari na idhini yako, nitenge na kufuru yoyote, hata ile ndogo kabisa.

KITUO CHA NNE: Yesu Anakutana na Mama yake.
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Ingawa kazi zote ambazo zinatokana na mapenzi Yangu zinaoneshwa kwa mateso makubwa, fikiria ikiwa yeyote kati yao amepata shida kubwa kuliko kazi hiyo ambayo ni yangu moja kwa moja – Kazi ya Ukombozi. Haupaswi kuwa na wasiwasi sana juu ya mateso. (1643).
Mtakatifu Faustina: Nilimuona Mama Bikira Maria (…), alifika karibu yangu (…) akasema maneno haya: Kuwa na ujasiri. Usiogope vikwazo dhahiri, bali yaangalie Mateso ya Mwanangu, na kwa njia hii utakuwa mshindi. (449).
Maria, Mama wa Huruma, uwe nami kila wakati, haswa katika mateso, kwa namna ile ile ambayo ulikuwepo katika njia ya Msalaba ya Mwanao.

KITUO CHA TANO: Simon wa Kirene Anamsaidia Yesu Kubeba Msalaba
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Ninaruhusu shida hizi ili kuongeza mastahili yake. Sitoi thawabu kwa matokeo mazuri bali kwa uvumilivu na ugumu unaofikiwa kwa ajili Yangu. (86).
Mtakatifu Faustina: Ee, Yesu wangu, hautoi thawabu kwa kufanikiwa kwa kazi, lakini kwa mapenzi mema na kazi iliyofanywa. Kwa hivyo, mimi nina amani kabisa, hata ikiwa yote niyafanyayo na kwa juhudi zangu zote yatapingwa au kukataliwa. Ikiwa nafanya yote yaliyo ndani ya uwezo wangu, mengine si kazi yangu. (952).

Ee Yesu, takasa nia zangu, ili kwamba kila wazo, kila neno, kila shughuli ifanywe kwa kukupenda wewe tu.

KITUO CHA SITA: Veronika Anapangusa Uso wa Yesu
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Tambua ya kuwa kila jambo jema ufanyalo kwa mtu mwingine, ninakubali kana kwamba umenifanyia. (1768).
Mtakatifu Faustina: Ninajifunza jinsi ya kuwa mwema toka kwa Yesu, Yeye ambaye ni wema wenyewe, ili niweze kuitwa binti wa Baba wa mbinguni. (669). Upendo mkubwa unaweza kubadilisha vitu vidogo kuwa vikubwa, na ni upendo tu ambao hutoa faida kwa matendo yetu. (303).
Bwana Yesu. Bwana wangu, fanya macho yangu, mikono yangu, mdomo wangu, moyo wangu… huruma. Nibadilishe niwe huruma yako.

KITUO CHA SABA: Yesu Anaanguka kwa Mara ya Pili.
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Sababu ya kuanguka kwako ni kwamba
unajitegemea sana na kuwa na utegemezi mdogo Kwangu. (1488). Lazima ujue kuwa wewe peke yako, huwezi kufanya chochote. (639). Huwezi hata kupokea neema yangu bila msaada wangu. (738).
Mtakatifu Faustina: Yesu, usiniache peke yangu (..). Unajua, Bwana, jinsi nilivyo dhaifu. Mimi ni fukara na mnyonge; Mimi si kitu chochote; itashangaza sana kama utaniacha peke yangu na mimi nikaanguka (1489). Kwa hiyo Ee Yesu, lazima usimame nami kama mama na mtoto asiye na msaada – na hata zaidi. (264).
Naomba nitegemee neema yako, Bwana, ili nisianguke kwenye makosa yale yale: na nikianguka, nisaidie kuinuka na kutukuza huruma yako.

KITUO CHA NANE: Yesu anawatuliza Wanawake wa Yerusalemu
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: O, jinsi gani Imani hai inavyonipendeza! (1420). Natamani kwamba wote mngekuwa na imani zaidi wakati huu wa sasa (352).
Mtakatifu Faustina: Mimi namwomba Bwana aimarishe imani yangu, ili kwamba katikamaisha yangu ya kila siku, nisiongozwe kwa matakwa ya kibinadamu, bali kwa yale ya Roho. O, jinsi gani mwanadamu anavutwa na mambo ya duniani! Lakini imani thabiti huiweka roho mahali pa juu na kuipa kazi ya matendo ya upendo. (210).
Bwana mwenye huruma, nakushukuru kwa Ubatizo Mtakatifu na neema ya imani. Ninakuita tena. Bwana, naamini, Ongeza imani yangu!

KITUO CHA TISA: Yesu Anaanguka Mara ya Tatu
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Fahamu ya kuwa vikwazo vikubwa zaidi dhidi ya utakatifu ni wasiwasi na kuvunjika moyo. Hivi vitakunyima uwezo wa kutenda kwa uadilifu (…). Mimi daima niko tayari kukusamehe. Kila uombapo msamaha, hutukuza huruma yangu (1488).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu wangu, licha ya neema zako. Ninaona na kuhisi taabu zangu zote. Mimi huanza siku yangu kwa vita na kuishia kwa vita. Mara tu ninaposhinda kikwazo kimoja, kumi zaidi huonekana kuchukua nafasi yake. Lakini sina wasiwasi, kwa sababu najua kwamba huu ni wakati wa mapambano, si amani. (606)
Bwana wa Huruma, ninakupa kila kitu ambacho ni mali yangu ya kipekee, yaani, dhambi na udhaifu wa kibinadamu. Nakusihi kwamba, taabu na udhaifu wangu vizamishwe kwenye huruma yako isiyoelezeka.

KITUO CHA KUMI: Yesu Anavuliwa Nguo
Mtakatifu Faustina: Yesu alisimama ghafla mbele yangu, akiwa amevuliwa nguo zake, mwili Wake umefunikwa na vidonda, macho Yake yakibubujika machozi na damu, uso Wake ulivyoharibika na kutemewa mate. Bwana Kisha akaniambia: “bibi harusi sharti afanane na Mchumba wake.”
Mtakatifu Faustina: Niliyaelewa maneno haya kwa kina sana. Hakuna nafasi ya kutia shaka hapa. Kufanana na Yesu lazima iwe kwa njia ya mateso na unyenyekevu (268).
Yesu, mpole na mnyenyekevu wa moyo, badili moyo wangu ulingane na moyo wako.

KITUO CHA NA MOJA: Yesu Anapigiliwa Msalabani
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Mwanafunzi wangu, uwe na upendo mkubwa kwa wale wanaokusababishia mateso. Wafanyie mema wale wanaokuchukia (1628).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu wangu, wewe wajua nguvu zinazohitajika kuishi kwa uaminifu, na bila kuathiriwa na wale ambao asili yetu inawakimbia, au kwa wale ambao, kwa makusudi au la, wametufanya sisi kuteseka. Kibinadamu, hii haiwezekani na hasa kwa nyakati hizi, Mimi hujaribu kumgundua Bwana Yesu ndani ya mtu kama huyu kwa ajili ya huyu Yesu, mimi hufanya kila kitu kwa ajili ya watu kama hao. (766).
O Upendo safi, utawale katika moyo wangu na uniruhusu nipende zaidi ya kile kipimo cha upendo wa mwanadamu. (328).

KITUO CHA KUMI NA MBILI: Yesu Anakufa Msalabani
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Haya yote ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Binti yangu, tafakari, kuhusu kile unachokitenda kwa ajili ya wokovu wao (1184).
Mtakatifu Faustina: Kisha nikamwona Bwana Yesu aliyepigiliwa msalabani. Na akiwa bado amejitundika kwa kitambo, nikaona umati wa watu waliosulubiwa kama yeye. Umati wa pili hawakuwa wamesulubishwa kwenye misalaba yao, bali walikuwa wanaishikilia imara katika mikono yao. Umati wa tatu hawakupigiliwa misumari kwenye misalaba yao wala kuishikilia imara katika mikono yao, bali walikuwa wakiiburuta na wamekata tamaa. Yesu Kisha akaniambia:
Yesu: Je, unaona nafsi hizi? Wale ambao ni kama mimi katika maumivu na dharau watakuwa kama mimi pia katika utukufu. Na wale ambao hufanana nami kidogo katika maumivu na dharau watapata dhawabu kidogo katika utukufu wangu. (446).
Ee Yesu, Mwokozi wangu, nifiche katika kilindi cha moyo wako ili nilishwe na neema yako, niweze kuwa wewe na uwezo kwa kuupenda msalaba na katika ushiriki wa utukufu wako.

KITUO CHA KUMI NA TATU: Yesu Anapokelewa Mikononi mwa Mama Yake
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Roho pendwa kwangu ni zile zinazoamini katika wema wangu na zenye imani kamili kwangu. Najaza imani yangu juu yake, na hutoa chote kile ambacho huombwa (453).
Mtakatifu Faustina: Mungu wa Huruma, naijongea Huruma yako, wewe tu ndiye wema yenyewe. Ingawa taabu yangu ni kubwa, na makosa yangu ni mengi, ninatumainia huruma yako, kwa sababu wewe ni Mungu wa huruma, na tangu mwanzo wa nyakati, haijawahi kusikika, wala mbingu au nchi, kwamba nafsi inayotumaini katika Huruma yako imekatishwa tamaa (1730)
Ee Yesu, zidisha ndani mwangu tumaini la huruma yako, ili daima na kila mahali nipate kuwa shahidi wa wema na upendo wako usio na mwisho.

KITUO CHA KUMI NA NNE: Yesu Anazikwa Kaburini
Maneno ya Yesu kwa Mtakatifu Faustina: Hauko bado katika nchi ya ahadi; enenda, kwa neema yangu, na upiganie ufalme wangu katika nafsi za wanadamu; pambana kama vile angefanya mwana mfalme; na kumbuka kwamba siku za Uhamishoni zitapita haraka, na pamoja nayo uwezekano wa kupata mastahili mbinguni. Natarajia kutoka kwako (…) idadi kubwa ya nafsi zitakazotukuza huruma yangu kwa milele yote (1489).
Mtakatifu Faustina: Ee Yesu, kila nafsi uliyonipatia, nitajaribu kuisaidia kwa sala na sadaka, ili neema yako iweze kufanya kazi ndani yake. O Mpenzi mkubwa wa roho, Yesu wangu, ninakushukuru kwa imani hii kubwa ya kudiriki kukabidhi nafsi katika huduma yetu. (245).
Bwana wa Huruma, nakuomba kwamba isipotee hata moja nafsi ya mtu ambayo umenipatia.

SALA BAADA YA NJIA YA MSALABA:
Ee Yesu wangu, tumaini langu la pekee, ninashukuru kwa kitabu hiki kikuu ambacho umekifunua mbele ya macho ya nafsi yangu. Kitabu hiki cha ajabu ni mateso uliyoyakabili kwa ajili ya upendo wako kwangu. Kutoka kitabu hiki nimejifunza jinsi ya kumpenda Mungu na roho. Hazina zisizoelezeka zimehifadhiwa ndani yake (…) Ee Yesu, jinsi gani roho chache zaelewa ulivyofia upendo (…). Heri kwa roho ile iliyoelewa upendo wa Moyo wa Yesu (304).

Pridaj komentár

Vaša e-mailová adresa nebude zverejnená. Vyžadované polia sú označené *