Sexe Model huren porn tube

Njia ya Msalaba – Catalina

UTANGULIZI

Kijitabu hiki ni sehemu ya mkusanyo mkubwa wa vitabu, ambavyo ni misemo ya Yesu na Bikira Maria kwa Catalina (Katya) Rivas. Vitabu hivi vyasadifu mafundisho na maisha ya kiroho ya Kikatoliki na waweza kuvipakua bila malipo kutoka wavuti ya “www.LoveAndMercy.Org” kwa ajili ya kujisomea na kuprinti. Watu wanashauriwa kurudufu maandishi haya bila kuyafanyia mabadiliko na kuyagawa katika kuungana na Papa Johani Paulo wa Pili katika Uinjilisha Mpya.

Vitabu hivi vya “Utetezi Mkuu wa Imani” (“The Great Crusade”) vimetafsiriwa pia kwa lugha ya Kihispaniola vikiwa na mafundisho na mwongozo wa kiroho kwa ajili ya utume wa Uinjilishaji Mpya, na msingi wake katika Maandiko Matakatifu na Katekesimu ya Kanisa Katoliki. Vitabu hivi vinaendelea kutafsiriwa katika kiingereza na lugha nyinginezo na kupewa ruhusa ya uchapaji na mamlaka rasmi za kanisa.

Utume wa Uinjilishaji Mpya (UUM) ni utume wa walei ulioanzishwa na baba Mtakatifu Yohane Paulo II katika kuwashirikisha kikamilifu wabatizwa wote kujikita na kujitoa katika kusambaza Habari njema ya Yesu kwamba alikufa na akafufuka kwa ajili ya wokovu wetu kutoka dhambini.

Tukiwa kama wakatoliki, tunajiweka kabisa chini ya Mafundisho ya Kanisa kuhusu ‘Uvuvio wa Binafsi’ kama inavoonekana katika Kanoni ya 66 na 67 katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki iliyochapwa mwaka 1994.

Canoni 66: “Mpango wa Kikristo wa wokovu, kwa kuwa ni agano jipya na Dhahiri, hautapita kamwe na hapatakuwa na ufunuo mpya bayana unaohusu watu wote kabla ya tokeo tukufu la Bwana wetu Yesu Kristo.” Ingawa ufunuo umekamilika, bado haujafafanuliwa kikamilifu. Ni juu ya Imani ya Kikristo kuufahamu kwa taratibu jinsi ulivyo karne hadi karne.

Canoni 67: Katika mfululizo wa karne kumekuwapo na ufunuo mwingine uliojulikana kama “watu binafsi” ambao baadhi umekubaliwa na mamlaka ya Kanisa. Ufunuo huo hausiani, wala hauwiani kwa vyovyote na amana ya Imani. Kazi yake siyo “kufanya vizuri zaidi au kukamilisha” ufunuo Dhahiri wa Kristo, bali kusaidia kuuishi kikamilifu zaidi katika kipindi fulani cha historia. Kwa kuongozwa na Mamlaka Rasmi ya Ufundishaji wa Kanisa, ufahamu wa waamini (sensus fidelium) hujua kupambanua na kupokea funuo hizo kile ambacho kinaunda mwito wa kweli wa Kristo na Watakatifu wake kwa Kanisa.

Imani ya Kristo haiwezi kupokea “funuo” ambazo zinajidai kupita au kusahihisha ufunuo ambao Kristo ni utimilifu wake. Jambo hili linahusika na dini fulani fulani zisizo za Kikristo na pia vikundi fulani vya kisasa ambavyo vinajijengea misingi yao katika “funuo” za namna hiyo.

Kama Yesu ameongea nawe moyoni kupitia usomaji wa kitabu hiki, tafadhali washirikishe wengine maneno haya wale watakaofungua mioyo yao kwa ajili ya utume wa walei wa Uinjilishaji Mpya. Mwite Roho Mtakatifu ili akuongoze na kukupa mapaji uanayohitaji kwa ajili ya kuongoka vyema na kuwapa pia wale utakaowashirikisha kijitabu hiki.

VITUO VYA NJIA YA MSALABA

Jiruhusu kuongozwa na hamu kuu kwamba roho zote zitajiosha ndani ya maji ya msamaha, na kwamba hisia za kujiamini na sio za woga zitakaa ndani yao, kwa sababu mimi ni Mungu wa Huruma na kwamba nipo tayari muda wote kuwapokea Moyoni Mwangu.

Unapofanya ninachokwambia, Nipo karibu yako. Utii wako utamaliza hamu yangu kuu ambayo ilikausha midomo yangu pale msalabani.

Nitakuwa nawe kila unapoyaita mateso yangu kwa upendo. Nitakuruhusu uungane nami katika mateso ambayo nilipitia katika bustani ya Getsemani nilipoziona dhambi za wanadamu.

Fikiria kila kitu nilichopitia katika kumkomboa mwanadamu, ili kuweza kutawala mioyo yao, ili kuwafanya waweze kuingia katika Ufalme wa Baba yangu.

Na sasa tuingie katika tafakari ya Mateso yangu… ambayo yanaendelea kumpa utukufu Mungu na utakatifu wa roho.

Tutembee pamoja katika Njia ya Msalaba.

KITUO CHA KWANZA

PILATO ANAMHUKUMUYESU AFE

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Kwa kuzungushiwa taji ya miiba, na kufunikwa na nguo ya zambarau, askari walinipeleka tena kwa Pilato. Bila kuona kosa la kuniadhibu, Pilato alikuwa anatafuta namna ya kuniachia huru. Katika hali ya kuhuzunisha niliyokuwa nayo, Pilato alinionesha kwenyekundi la watu. Alipendekeza niwe huru na kumwadhibu Baraba, aliyekuwa mwizi na muuaji mzoefu. Watu wakapiga kelele: “Msulubishe na umwache Baraba huru.”

Roho zinazonipenda, angalieni jinsi nilivyolinganishwa na Mkosaji. Jinsi walivyonidharau na kunishusha chini zaidi hata ya Mkosaji Mkubwa. Tafakari kwa muda juu ya kifoshahidi cha moyo wangu kisichoweza kuongelewa: Moyo wangu unadharauliwa zaidi ya moyo wa Baraba. Mimi nimedharauliwa zaidi, na kuhukumiwa kifo kama Mkosaji ninayejulikana. Pilato ametoa hukumu. Watoto wangu wadogo, fikirieni kwa makini jinsi Moyo wangu ulivyoteseka…

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA PILI

YESU ANAPOKEA MSALABA

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Tuendelee, wanangu wapendwa. Mnifuate kuelekea Kalvario, Nimeelemewa na uzito wa msalaba…

Wakati moyo wangu umejaa huzuni kwa kumpoteza Yuda, wauaji wakatili, wasiojali mateso yangu, wanaupagaza msalaba katika mabega yangu yaliyojaa vidonda. Kupitia msalaba nimekamilisha fumbo la ukombozi wa ulimwengu.

Tafakarini mateso yangu, enyi malaika wa mbinguni. Tazama Muumba wa maajabu yote; Mungu ambaye Malaika wote mbinguni wanamwabudu; Mungu anayeelekea Kalvario akiwa amebeba msalaba wa mbao takatifu; Mungu anayeenda kuvuta pumzi yake ya mwisho.

            Tafakari mateso yangu enyi mnotaka kunifuata. Mwili wangu ulioharibiwa na mateso makali, ulitembea kwa ulegevu, mwili uliooshwa kwa jasho na damu…

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA TATU

YESU ANAANGUKA KWA MARA YA KWANZA

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Nateseka pasipo kuonewa huruma na watu katika machungu yangu. Nitembeapo, hakuna hata mmoja toka kwenye kundi la watu anioneaye huruma. Nimezungukwa na mbweha wenye njaa, wanaotaka kunifanya kitoweo. Mapepo yote yanatoka kuzimu kutilia nguvu mateso yangu.

Uchovu nilio nao ni mkubwa mno na msalaba pia ni mzito sana, kiasi kwamba nimeanguka katikati ya safari. Katika unyama mkuu, askari wananilazimisha kuunyanyua msalaba. Askari mmoja ananishika kwa mkono na mwingine anabandua kwa nguvu nguo yangu iliyogandamana na madonda yangu, anayaamsha tena madonda yangu… Tena askari mwingine ananikaba shingoni na mwingine nywele zangu. Kundi la Maaskari wananipiga ngumi, wengine wananichapa kwa mijeledina viboko mwili wangu wote. Msalaba unaanguka juu yangu na kutokana na uzito wake unanisababishia majeraha mapya. Uso wangu unakandamizwa kwenye mawe yalioyoko njiani. Damu inatiririka toka usoni na kuziba macho yangu ambayo yamekaribia kufifia. Vipigo nilivyovipata vimesababisha macho yangu kuvimba. Vumbi na matope vinachanganyika na damu na kunifanya nionekana mkosefu mkubwa.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA NNE

YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Endelea nami kwa kitambo kidogo, na hatua chache mbele utaniona mbele ya Mama yangu. Moyo wake unachomwa kwa maumivu. Anakuja kukutana nami kwa sababu mbili. Moja kujipa nguvu ya kuteseka mbele ya Mwanae na Mungu. Na kwa roho yake ya ujasiri, kumtia motisha mwanae ili asonge mbele na kazi yake ya Ukombozi.

Fikiria ushahidi wa Mioyo hii miwili. Ambacho mama yangu anakipenda sana ni Mwanae… Hawezi kupunguza maumivu yangu na anatambua kuwa kuja kwake kuniona kunaongeza maumivu yangu zaidi. Hata hivyo, uwepo wake unaniongezea nguvu ya kutimiza mapenzi ya Baba yangu.

Ninampenda Mama yangu zaidi ya vyote kati ya vilivyopo duniani, na najua sitaweza kumtuliza. Hali mbaya Anayoniona nayo Inamsababishia mateso makubwa moyoni kama ya kwangu. Anaruhusu machozi yatoke. Anapokea moyoni mwake kifo ninachokitesekea mwilini. O, jinsi gani macho yangu na yake yanatazamana! Hatuongei neno lolote, lakini mioyo yetu inasema vitu vingi katika hali hii ya maumivu.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA TANO

SIMONI WA KIRENE ANAMSAIDIA YESU MSALABA

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Niko njiani kuelekea Kalvario. Wauaji wasiopenda kuniona nakufa kabla ya kufika mwisho wa safari, wanatafuta mtu wa kunisaidia kubeba msalaba, wanamkamata Simoni aliye jirani na msalaba ili anisaidie kuubeba. Simoni ananisaidia kubeba sehemu tu ya msalaba lakini mzigo wa msalaba wangu bado ni kazi kuuhimili.

Kuna roho zinazonifuata ninapoelekea Kalvario. Ijapokuwa wamekubali kunisaidia kuubeba msalaba lakini wana wasiwasi juu ya faraja na starehe. Wapowengine wengi wamekubali kunifuata; akilini mwao bado wamekumbatia Maisha mazuri. Wameweka kipaumbile kwenye ubinafsi nahivyo wamejikuta wakijikwaa na kuudondosha msalaba wangu pale unapokuwa mzito kwao. Wanatazama kuteseka kama chaguo la mwisho kuwezekana. Wanalinganisha mateso na ufukara, udhalilishaji na uchovu. Wanawakumbuka na wanawahurumia wale waliowaacha,wanaamua kujitafutia wenyewe baadhi ya vitulizo na starehe.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA SITA

VERONIKA ANAPANGUSA USO WA YESU

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Zipo roho nyingi zinazovutwa na tamaa ya ukombozi. Ni uvuvio wa upendo kutokana na mtazamo wa wale nilioteseka kwaajili yao ili waamue kunifuata mimi katika njia ya Kalvari. Wanakumbatia maisha ya ukamilifu na kujitolea wao wenyewe kwa huduma yangu. Hunisaidia sio tu kubeba sehemu ya msalaba bali huubeba wote. Matamanio yao ni kunifariji mimi na kunipatia mapumziko. Wanajitoa wao wenyewe kwaajili ya utashi wangu, ili kutafuta kile kiwezacho kunifurahisha. Hawafikirii kuhusu tuzo au zawadi ziwangojeazo, wala hawajali uchovu wa mateso yajayo. Wao hujali tu ule upendo ambao wanaweza kunionyesha, na faraja wanayoweza kunipatia…

Wanakubali kwa kujitoa kikamilifu na dhahiri msalaba unaojionyesha kama mateso. Pia wanapokea msalaba uliofichika katika kazi kinyume na maelekeo yao na uwiano mdogo wa uwezo wao. Pia wanapokea msalaba wa upweke- msalaba wa ukosekanaji wa watu wanao-wazunguka.

Oh! Hizi ndizo roho ambazo kweli zinabeba msalaba wangu, wanauabudu. Wanatumia fursa ya msalaba wangu kunitukuza. Wanafanya hivi bila kutafuta manufaa au malipo yoyote isipokuwa upendo wangu. Hao ndio wanaonijali na kunitukuza.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, Utuhurumie.

KITUO CHA SABA

YESU ANAANGUKA MARA YA PILI

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Mtazame Simoni aliye nyuma yangu; ananisaidia kuchukua msalaba. Ni mtu asiye na nia njema; ni mamluki kwakuwa ananisaidia na kushiriki uzito wa msalaba kwasababu amelazimishwa kufanya hivyo. Kwa sababu hiyo, akihisi kuchoka anaacha uzito wote wa msalaba unielemee. Na hivyo kupelekea kuanguka kwangu mara ya pili.

Baba yangu huwatuma malaika kunisaidia. Wananisaidia kubaki na fahamu zangu za kibinadamu niapoanguka. Vita yangu ni lazima iendelee hadi muda muafaka ili kusudi roho nyingi zisipotee.

Natembea juu ya mawe yanayoharibu miguu yangu. Ninapojikwaa na kuanguka, ninatazama katika umati ili nione nyuso ndogo za upendo, zinazoungana na maumivu yangu, hatahivyo…. Sioni mtu anayenihurumia.

Wanangu, ninyi mnaofuata nyayo zangu hamtaacha misalaba yenu hata kama inaonekana kuwa mizito sana? Fanyeni hivyo kwaajili yangu. Katika kubeba misalaba yenu, mtanisaidia mimi kubeba wangu, na katika njia ngumu, mtamkuta Mama yangu na roho takatifu ambazo watawapa msaada na faraja.

+ Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA NANE

YESU ANAZUNGUMZA NA WANAWAKE

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Enyi mabinti wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni wenyewe na watoto wenu. Kwa kuwa siku zinakuja ambapo watasema, “wamebarikiwa tasa na matumbo yasiyozaa, na matiti yasiyonyonyesha kamwe.” Tazama, kama huoni matokeo ya mateso yako, kujinyima kwako, au unayaona baadaye, uwe na hakika kuwa hayakuwa bure au bila matunda.

Roho inayopenda kweli, haihesabu ni kwa kiasi gani imeteseka au kufanya kazi, wala haitafuti zawadi. Inatafuta kile tu ambacho inaamini kinamtukuza Mungu … Kwake si mahangaiko wala mateso yanayochosha. Haterereki wala hachoki bali hubaki tulivu na katika amani. Inapokutana na vikwazo au inaponyanyasika, haijali. Chanzo pekee cha matendo yake ni upendo, na upendo haujali matokeo. Roho hizi ambazo hazitafuti manufaa huchochewa na upendo. Hutamani kushiriki katika utukufu wangu pekee, kuniliwaza, na kunisaidia nipumzike. Kwa sababu hiyo zimechukua msalaba wangu na uzito wote amabao utashi wangu unataka waubebe.

+ Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

YESU ANAANGUKA MARA YA TATU

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Unyong’onyevu unaniingia kwani ni vigumu hata kutembea. Miguu yangu inatiririka damu kwasababu ya mawe njia yaliyokatakata miguu yangu… naanguka mara ya tatu. Mara tatu nimeanguka njiani. Ya kwanza ni kwaajili ya kuwaonesha wadhambi waliozoea kutenda dhambi ili waongoke na waimarike hata kama wameanguka dhambini. Kuanguka kwangu mara ya pili ni kwaajili ya zile roho zinazoshindwa kwa sababu ya ulegevu au zile ambazo zimepofushwa kwa huzuni na mahangaiko, ili wanyanyuke na kuendelea na kwa ujasiri katika njia ya fadhila. Kuanguka kwangu mara ya tatu ni kwaajili ya zile roho zinazo jiondoa katika dhambi saa ya kufa….

Wanangu, niiteni kwa jina langu,kwani Yesu lina maana ya kila kitu. Nitawaosheni miguu, ile miguu iliyopitia njia ya utelezi unaopelekea majeraha katika miguu yao kwa kujikwaa katika miamba. Nitawafuta machozi, nitawaponya, na kuwabusu. Hivyo mtabaki wenye afya na hamtafahamu njia nyingine isipokuwa ile iongozayo kwangu.

Roho ninazozimiliki, hazimsikilizi adui wetu katili. Mara tu unapohisi neemavita vinapoanza, njoo katika moyo wangu. Hisi na tazama moyo wangu jinsi unavyotiririshatone la damu kwaajili ya roho yako. Nawe utakuja kwangu. Utafahamu nilipo: kwa mwavuli wa Imani… Nyanyua juu kitambaa hiki kwa ujasiri mkubwa na unishirikishe masikitiko yako yote, mahangaiko yako, na maanguko yako yote… sikiliza maneno yangu kwa heshima na usiogope kwaajili ya yaliyopita. Moyo wangu umejizamisha katika kina kirefu cha huruma yangu na upendo wangu.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA KUMI

YESU ANAVULIWA NGUO

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Tazama watu wakatili hawa walivyonizunguka. Baadhi yao wamesukuma msalaba wangu na kuuangusha chini; wengine wanafanya kazi ya kuchana mavazi yangu yaliyogandamana na madonda wanayaamsha tena maumivu huku damu zikivuja.

Tazama, wanangu wapendwa, ni aibu kiasi gani na mahangaiko nimeteseka kwa kudhalilishwa kiasi hiki kati ya kundi lile… Roho yangu inateseka sana!

Wauaji wanachana kanzu yangu na kuipigia kura, kanzu ambayo mama yangu alinivisha kwa kunijali kipindi nilipokuwa mdogo, na kukua nayo. Ni uchungu mkali kiasi gani Mama yangu anaousikia anapotafakari tendo hili!

Tafakari kwa muda mikono na miguu hii iliyojaa damu… Mwili huu ulio tupu, uliojaa madonda, pamoja na uchafu, na damu. Uchafu… Kichwa changu kimetobolewa na miiba mikali, kimezongwa na jasho, kimejaa vumbi, na kufunikwa na damu…

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA KUMI NA MOJA

YESU ANATUNDIKWA MSALABANI

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Sasa ndio muda wauaji wananyoosha mikono yangu juu ya Msalaba. Wanavuta mikono yangu ifike mahali palipo na matobo yaliyoandaliwa juu ya msalaba. Mwili wangu wote umechoshwa, unaning’inizwa upande hadi upande. Taji la miiba linapenya ndani kabisa ya kichwa changu. Sikiliza mshindo wa kwanza wa nyundo ambao unapigilia msumari mkono wangu wa kulia… Sauti ya mvumo huo unajirudia katika kina cha dunia. Sikiliza tena… Sasa wanapigilia msumari mkono wangu wa kushoto. Mbele ya macho yao, mbingu zatetemeka, na malaika wanasujudu kifudifudi. Ninaweka kimya kikuu. Midomo yangu isilalamike wala kuhuzunika kwa sababu ya maumivu hayo lakini machozi yangu yachanganyike na damu inayofunika uso wangu.

Baada ya kutundika mikono yangu, wanavuta miguu yangu kwa ukatili mkubwa wawezavyo. Madonda yangu yanaamka, neva za viganja na mikono yangu zianapasuka. Mifupa yangu inavunjika kutoka kwenye maungio yake… Maumivu ni makali mno! Miguu yangu imepigiliwa misumari na damu yangu inailowanisha ardhi.

Mtafakari Yesu aliye juu ya msalaba, ambaye hawezi kusogea hata kidogo… nipo mtupu- sina heshima, sina uhuru… wamechukua kila kitu kutoka kwangu! Hakuna anayenionea huruma na kunipa pole kwa maumivu yangu! Nimepata mateso, maumivu, na mzaha.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie. 13

KITUO CHA KUMI NA MBILI

YESU ANAKUFA JUU YA MSALABA

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Mwanangu umesikia na kuona mateso yangu; nisindikize hadi mwisho na kushiriki maumivu yangu.

Msalaba wangu sasa umesimamishwa. Hii ndiyo saa ya ukombozi wa dunia! Kundi linanitazama kwa dharau… lakini roho zinashauku na mimi na zinanipenda. Msalaba huu, ambao mpaka sasa ni chombo cha mateso ambamo wahalifu wanauawa, kuanzia sasa unakuwa mwanga na amani ya Dunia. Nimetolea kifo changu kwa Baba yangu kwa ajili ya roho zilizokufa ili ziwe na uzima. Kwa kilio cha mwisho pale msalabani, nimeukumbatia ubinadamu: wa-zamani, wa-sasa, na ujao.

Wanangu, hakuna misalaba ya utukufu duniani. Misalaba imefunikwa mafumbo, giza na maovu. Imefunikwa na mafumbo kwa sababu hamyaelewi; imefunikwa na kiza, kwa sababu inachanganya akili; na imefunikwa na uovu kwa sababu inagusa sehemu tusizopenda ziguswe.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA KUMI NA TATU

YESU ANASHUSHWA CHINI YA MSALABA

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Hakuna muda wa kulaumu wala muda wa kuchelewa. Ninawaambia kwamba si tu nilibeba msalaba wa mbao ulioleta utukufu, lakini, cha muhimu zaidi, nilibeba msalaba usioonekana lakini wa daima ulioundwa na misalaba ya dhambi zenu. Kwa ajili ya mateso yenu yote, ndio kielelezo cha masikitiko yangu. Niliteseka si tu kuwaletea wokovu, lakini pia kwa ajili ya mateso yenu ya leo. Tazameni pendo linaloniunganisha mimi na ninyi; katika hilo muwe imara katika utashi wangu Mtakatifu. Muungane nami, mkitazama jinsi gani nilitenda mateso yasiyo na mwisho.

Msalaba ni kielelezo. Nimeubeba kwa upendo mkubwa, kwa manufaa ya wote. Nimeteseka mateso makali sana ili kila mmoja awe na furaha pamoja nami. Lakini leo, ni wangapi wanaoamini kwa Yule aliyewapenda kweli na anayewapenda? Nitafakarini Mimi katika uso wa Kristo ambaye analia na kuvuja damu. Kwa damu hiyo na kwa njia hii dunia imenipata.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA KUMI NA NNE

YESU ANAZIKWA KABURINI

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Nimeuumba ulimwengu na mti uliotumika kutengenezea msalaba wangu. Niliumba na kupalilia vichaka ambavyo vilikuja kutoa miiba kwa ajili ya taji langu la kifalme. Niliweka chini ya ardhi vyuma (misumari) ambavyo vingepigiliwa katika mikono yangu. O! Ni fumbo la upendo lisiloweza kueleweka! Nimetengeneza Kiota kwa ajili ya ndege, pango kwa ajili ya wanyama wa porini, Jumba la kifalme kwa ajili ya matajiri, nyumba kwa ajili ya wafanyakazi, kitanda kwa ajili ya watoto, nyumbani/makao kwa wazee. Nilipokuja mwenyewe kutembelea ardhi yangu, hapakuwa na mahali pa mimi kupumzika hapa ulimwenguni. Kulikuwa na baridi, dunia iliyopoa wakati nilipokuja kama mtu. Nilikuja kwa wanadamu lakini wanadamu hawakunitambua. Hapakuwa na chumba kwa ajili yangu … Na sasa?…

Watoto wangu, maskini wadhambi! Msijiweke mbali nami. Ninawasubiri mchana na usiku katika tabernakulo. Sitawalaumu kwa sababu ya makossa yenu; sitawatupia dhambi zenu katika nyuso zenu. Nitakachofanya ni kuwaosha na damu yangu itokayo katika madonda yangu. Msiogope, njooni kwangu. Hamjui ni kwa kiasi gani nawapenda.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

KITUO CHA KUMI NA TANO

UFUFUKO WA YESU

+ Ee Yesu Tunakuabudu, na Tunakusifu, kwa kuwa Umeukomboa Ulimwengu kwa Msalaba wako Mtakatifu

Ijumaa kuu ilifuatiwa na utukufu wa Jumapili ya Ufufuko. Ni damu yangu iokoayo inayoilowesha ardhi iliyokauka na kuwa jangwa katika ulimwengu wa roho. Na damu hii itaendelea kutiririka juu ya uso wa dunia kama kuna mwanadamu yeyote wa kuokoa. Sijafa juu ya Msalaba, na kupitia maelfu ya mateso ili kuongeza watu motoni, bali kuongeza idadi ya watu mbinguni waliochaguliwa.

Nasema tena, Wanangu, maskini wadhambi! Msijiweke mbali nami. Ninawasubiri mchana na usiku katika tabernakulo. Sitawalaumu kwa sababu ya makosa yenu; sitawatupia dhambi zenu katika nyuso zenu. Nitakachofanya ni kuwaosha na damu yangu itokayo katika madonda yangu. Msiogope, njooni kwangu. Hamjui ni kwa kiasi gani nawapenda.

Njooni kwangu, watoto wangu. Njooni kwangu. Mimi na Bwana wenu ninayewasubiri katika Tabernakulo. Kwa hakika nipo mzima katika Mwili, Damu, Roho na Umungu. Unataka kunifahamu? Njoo na utumie muda wako na mimi. Ninawapenda, watoto wapendwa.

+Ee Yesu, Mtiifu, mpole na Mnyenyekevu wa Moyo, utuhurumie.

Pridaj komentár

Vaša e-mailová adresa nebude zverejnená. Vyžadované polia sú označené *