Sala ya kuomba maombezi ya Mtakatifu Padre Pio
Ee Yesu, uliyejaa neema na upendo, ukijitoa sadaka kwetu, hata kufa msalabani. Nakusihi kwa unyenyekevu unijalie neema zako kwa maombezi ya mtumishi wako, Mt. Pio wa Pietrelcina. Alishiriki kwa ukarimu mateso yako, akakupenda sana na kufanya kazi kwa uaminifu kabisa kwa ajili ya utukufu wa Baba yako wa Mbinguni na kwa ajili ya wokovu wa watu.
Kwa hiyo nakusihi kwa matumaini, unijalie kwa maombezi yake, neema ya ………………….. ambayo naihitaji Sana.
Atukuzwe Baba……………………(Mara 3).