Sala ya kuombea familia
Ee Mtakatifu Maximilian Kolbe, uliyetoa maisha yako ili familia isimkose baba na mume. Kwa kusukumwa na upendo kwa jirani ulikubali kufa shahidi kulinda umoja wa wanafamalia. Utufundishe sisi nasi kutambua kuwa, maisha ya familia yana thamani katika sadaka zetu pia.
Kama ulivyogundua ndani ya Mama Bikira Maria, mfereji wa neema zilizokuimarisha wewe kuwa mwaminifu kwa mwanaye, utusaidie nasi pia tufurahi naye, yeye aliyepewa kwetu kama Mama yetu pale Msalabani.
Mtakatifu Maximilian Kolbe, uwe nasi tunapoomba kwa ajili ya hitaji maalum la familia yetu (Taja ombi hapa). Amina.